TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA KINONDONI
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo :-
1. DEREVA II – NAFASI 10.
SIFA:
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II.
KAZI NA MAJUKUMU:
i) Kuendesha magari ya abiria na malori,
ii) Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa magari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
iii) Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
iv) Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-Book” kwa safari zote.
NGAZI YA MSHAHARA - TGOS. A
2. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III - NAFASI 4
SIFA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
KAZI NA MAJUKUMU.
Katibu Mahsusi Daraja la III atapagiwa kufanya kazi katika Tyiping Pool au chini ya Katibu Mahsusi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye ofisi ya Mkuu wa sehemu au kitengo.
i) Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
ii) Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
iii) Kusaidia kutunza taarifa aukumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
iv) Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v) Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
vi) Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo,na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
vii)Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. B
3. MTENDAJI WA MTAA II – NAFASI 55
SIFA
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha IV au VI aliyehitimuStashahada (DIPLOMA) katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikakali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
i) Katibu wa Kamati ya Mtaa;
ii) Mtendaji Mkuu wa Mtaa;
iii) Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
iv) Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
v) Msimamizi wa Utekelezeji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa;
vi) Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
vii)Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa;
viii) Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
ix) Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa; na
x) Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. C
MASHARTI YA JUMLA:
· Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo;-
i) Nakala za Vyeti vya Mwombaji vilivyothibitishwa,
ii) Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae),
iii) Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.
· Kila mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka 18 – 45
· Waombaji wenye Sifa Pungufu au zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.
· Watumishi waliopunguzwa kazi/kufukuzwa kazi Serikalini hawashauriwi kuomba.
· Waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitishia barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa
· Barua ambazo hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu (i – iii) hazitashughulikiwa.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA YA KINONDONI
S. L. P. 31902
2BARABARA YA MOROGORO,
14883 DAR ES SALAAM.
TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI:
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28.11. 2014 saa 9.30 Alasiri
............................
Eng. Mussa B. Natty
MKURUGENZI WA MANISPAA
KINONDONI
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA KINONDONI
Reviewed by Women4WomenTz
on
9:29:00 PM
Rating: