Tanga Women Gala 28/5/2016
Karibu Ukutane na Wahamasishaji mbalimbali, Women For Women Tanzania ina wataalam wa Masoko (Marketing) ya ndani na nje ya nchi, ambao ukikutana nao watakusaidia Kupata/kuongeza masoko ya bidhaa zako kitaifa na Kimataifa
Kwa wale ambao hawajaziona fursa na kuzifikia ndoto zao waje wakutane na Mjasiriamali ESTHER MELLA, aliyeamua kustaafu ajira ya Serikali na kujiajiri binafsi akiwa chini ya miaka 40. Alikuwa ni Lecture wa Chuo kikuu cha kimataifa UDOM na sasa amejikita kwenye ajira binafsi
Akiwa anaongea/nawafundisha Ujasiriamali amekuwa ni hamasa kubwa kwa Watu wa jinsia zote na Rika zote. Amefanikiwa kubadilisha mitazamo hasi na kuifanya Chanya, shuhuda zake zimesaidia kuwapa mtaji wa mawazo yenye mafanikio.
Aliamua kustaafu ajira akiwa na Umri wa miaka 40 tu, tena aliiacha ajira yenye sifa akafuata ajira yenye maendeleo na heshima, na sasa anajivunia sifa na mafanikio.
Ni Mke na Mama wa familia, njoo akusaidie namna ya kufanikisha ndoto zako na kukutoa kwenye utegemezi na kutokujiamini, zaidi atakuelimisha namna ya kuifanya Jamii nzima inayokuzunguka iwe inajitegemea badala ya kuishi kitegemezi.
Mahali ni Hoteli ya RIGO NAIVERA, ukumbi wa kifahari na wa kisasa, ambapo tutashiriki chakula cha jioni na Mh. Mussa Mbarouk Mbunge wa Tanga Mjini pamoja na Mkewe Bi Rukia, pia atakuwepo mwanamuziki Mkongwe na Mahiri Bi Mwanaheri. Njoo ukiwa umependeza sababu ni siku yako ya kukutana na kupata kumbukumbu ya picha na wanawake wenzio tofauti tofauti wenye maendeleo na walio maarufu na wenye hamasa kutoka nje na ndani ya Mkoa wa Tanga. Watakuwepo viongozi wa Kiserikali na Kidini pia.
Kutakuwa na Burudani mbalimbali zikiongozwa na kikundi maarufu cha Taarab cha hapahapa Tanga.
Ticket zinapatikana kwa mawasiliano yafuatayo:
1. Bi Rukia, Mke wa Mheshimiwa Musa Mbarouk Mbunge wa Tanga - 0652 522 228
2. Mama Mchungaji Happiness Titu. Bombo hospital - 0712 443 846
3. TCCIA Tanga kwa Anna - 0712 999 947
4. Naivera Hotel
5. Bi Ghaitha, barabara ya 18 - 0654620148
Tanga Women Gala 28/5/2016
Reviewed by Women4WomenTz
on
12:00:00 PM
Rating:
She is amazing, people need to learn from these intellectuals
ReplyDelete