Rais wa Brazil Mwanamama Dilma Rousseff kikaangoni
Bunge la Seneti Brazil limepiga kura kuamua kuidhinisha kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo Dilma Rousseff.
Atasimamishwa kazi ya urais kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litakagua tuhuma zinazomkabili.
Masenata 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwana imani katika kikao cha zaidi ya saa 20
Makamu wa rais Michel Temer sasa ndio atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Rousseff inaendelea.
Rousseff alichukua hatua ya mwisho kujiokoa kwa kukataa rufaa katika mahakama ya juu zaidi nchini humo kusitisha kura hiyo, lakini hatua hiyo ilipingwa.
Rais wa Brazil Mwanamama Dilma Rousseff kikaangoni
Reviewed by Women4WomenTz
on
8:18:00 AM
Rating:
No comments