UWASILISHAJI WA TAARIFA ZA MAKAMPUNI YANAYOTOA MIKOPO KWA KUTUMIA MITAJI BINAFSI



Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kama Mmamlaka ya Utoaji wa Leseni za Biashara kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, iliandaa miongozo ya usimamizi wa Biashara ya kutoa mikopo kwa kutumia mitaji binafsi. Kampuni zilizopewa leseni za biashara ya aina hii zilisaini masharti ya kufanya biashara hiyo, ambayo yanamtaka mwombaji kuwasilisha tarifa za mikopo iliyotolewa kila baada ya miezi minne na pale watakapohitajiwa kufanya hivyo na Mamlaka ya Utoaji wa Leseni hizo.  Wamiliki wa makampuni yenye leseni za kutoa mikopo kwa kutumia mitaji binafsi, mnakumbushwa kuwasilisha tarifa kupitia anuwani na barua pepe iliyopo hapa chini kama ilivyokubalika katika masharti ya leseni zenu. Kutowasilisha tarifa hizo kutasababisha kunyang’anywa leseni ya biashara na kufungiwa kufanya biashara hii. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA:- Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, NSSF Water Front, Ghorofa ya 1, 35 Barabara ya Edward Sokoine, S. L. P 9503, 11469 DAR ES SALAAM. Simu: Na.+255 -2-2129111/8 +255 -22- 2129109 Fax:+255-22-2125832 Email: ps@mit.go.tz nakala:-dtm@mit.go.tz Website- www.mit.go.tz IMETOLEWA NA KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
UWASILISHAJI WA TAARIFA ZA MAKAMPUNI YANAYOTOA MIKOPO KWA KUTUMIA MITAJI BINAFSI UWASILISHAJI WA TAARIFA ZA MAKAMPUNI YANAYOTOA MIKOPO KWA KUTUMIA MITAJI BINAFSI Reviewed by Women4WomenTz on 5:17:00 AM Rating: 5

No comments