Wanawake shupavu waafrika



Hii ni kutokana na mtandao wa BBC SWAHILI kwa mwaka huu wa 2012. Nategemea mpaka miaka mitano ijayo namimi nitakuwepo kwenye hii list yao. embu soma wasifu wao uniambie je kwa hiyo miaka mitano siwezi fikia katika hizi namba tano?

Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika. Alichaguliwa tarehe kumi na tano mwezi Julai baada ya kinyang'anyiro kikali kati yake na mwenyekiti wa zamani Jean Ping. Bi Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka 63, ni mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo.

Ngozi Okonjo-Iweala, waziri wa fedha wa Nigeria. Bi Okonjo-Iweala, mwenye umri wa miaka 58, ameshikilia nyandhifa mbalimbali za kimataifa, katika sekta ya fedha .Aliheshimika sana wakati akiwa mkurugenzi mkuu katika benki ya dunia kwa miaka mitatu, kabla ya kushindana katika kinyang'anyiro kuwa rais wa benki hiyo.

Fatou Bensouda, mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC. Bensouda mwenye umri wa miaka 51, aliteuliwa katika wadhifa huo mwezi Juni mwaka huu na kuchukua nafasi ya Luis Moreno-Ocampo kutoka Argentina. Kabla ya hapo Bensouda alikuwa naibu mwendesha mkuu wa mashtaka tangu mwaka 2004.


Ellen Johnson-Sirleaf, rais wa Liberia ana umri wa miaka, 72 na alitajwa kama mshindi wa tatu wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Tuzo hiyo imetolewa miaka sita baada ya yeye kuchaguliwa rais wa Liberia na kumfanya kuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika.
 
Joyce Banda, rais wa Malawi. Bi Banda mwenye umri wa miaka 62, amefannya jambo la kihistoria kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo. Pia yeye ni mwanamke wa pili kuongoza nchi ya ya kiafrika. Anaheshimika kakam mwanaharakati wa haki za wanawake.



Wanawake shupavu waafrika Wanawake shupavu waafrika Reviewed by Women4WomenTz on 8:43:00 AM Rating: 5

1 comment